ads

Breaking News

Ben Pol aeleza kwanini hataki kuonekana na mpenzi wake kila wakati

Ben Pol
Ben Pol amesema ataamua kutembea kila sehemu na mpenzi wake baada ya kuona anakaribia kufunga naye ndoa.
Ben Pol ameiambia Bongo5 kuwa, kitu anachoogopa ni kuonekana mara kwa mara na mtu halafu siku chache watu wasikie wameachana.
“Kusema ukweli nahisi bado,” amesema. “Unajua mpaka uanze kutembea na mtu kwenye public mpaka ujiridhishe vitu fulani fulani na labda muwe kuna hatua fulani mmefika. Uchumba nini ndoa, sio unatembea na mtu na kumuonyesha kumbe mna migogoro. Kwahiyo lazima vitu muhimu vifanyike kwanza, mauchumba na pete na baadaye ndoa inakaribia ndio mnaweza kufanya hivyo,” ameongeza Ben Pol.

No comments