ads

Breaking News

Jennifer Lopez kukabiliwa na kifungo cha miaka 2 jela kwa show yake ya mitego ya kimapenzi mbele ya waziri mkuu wa Morocco

Jennifer-Lopez3Jennifer Lopez anaweza kukabiliwa na kifungo kwa kutumbuiza nusu uchi na kwa mitego lukuki ya kimapenzi mbele ya waziri mkuu wa Morocco.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 45 alitumbuiza mjini Rabat kwenye Mawazine World Rhythms International Music Festival na waziri mkuu Abdelilah Benkirane hajafurahishwa.
Utumbuizaji wa Jlo ulikuwa pamoja na kuinama na kuonesha makalio yake yanayovutia huku akiwa amevaa nguo zinazoonesha ndani na kwa jinsi alivyokuwa akizungusha kiuno chake jukwaani, wanaume walipata shida!
Jennifer-Lopez2
Waziri mkuu, Benkirane ameielezea show ya Jenny kwenye tamasha hilo, May 29 kama isiyokuwa na ‘staha’, yenye ‘uchokozi’ na ya ‘aibu kubwa.’
Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari la BBC, waziri mkuu huyo ameitaka mamlaka husika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya ukiukaji huo wa maadili.
Kama mama huyo wa watoto wawili akishtakiwa, atakabiliwa na kifungo cha miaka miwili jela.
Jennifer-Lopez
Waziri huyo mkuu pia alisema show hiyo iliyooneshwa kwenye TV ilikiuka sheria za nchi yake na imewadhalilisha wanawake.
Wiki iliyopita, waziri wa mawasiliano wa Morocco alikosolewa vikali kwa kuruhusu show hiyo iruke kwenye TV na amekuwa akishinikizwa ajiuzulu.

No comments