ads

Breaking News

Rapper tajiri zaidi si Dr. Dre…. ni Diddy – Forbes!


2ee440be-dc68-4fef-b5a0-06b23fb17f74

Dr. Dre si rapper tajiri zaidi kama wengi tulivyokuwa tukifahamu baada ya deal la Beats By Dre na Apple!


Diddy ndiye amechukua nafasi ya kwanza kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na Forbes ya wasanii wa hip hop wenye fedha zaidi duniani.
Diddy ana utajiri ufikio dola milioni 735 uliotokana na si muziki peke yake lakini riba zake kwenye makampuni kibao. Anamiliki na kushikilia hisa kwenye kampuni yake ya nguo ya Sean John pamoja na maji ya kunywa ya Aquahydrate.
Dr. Dre, aka Andre Young, amekamata nafasi ya pili kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 700. Fedha zake nyingi zimetokana na mauzo ya kampuni yake ya Beats Electronics kwa Apple mwaka jana. Dre alikuwa anamiliki asilimia 25 ya kampuni hiyo na aliingiza dola milioni 500.
Jay Z amekamata nafasi ya tatu kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 500. 50 Cent na Birdman wamemalizia nafasi za mwisho kwa utajiri wa dola milioni 155 na milioni 150.
1. Sean “P. Diddy” Combs – $735 million
2. Andre “Dr. Dre” Young – $700 million
3. Shawn “Jay Z” Carter – $550 million
4. Curtis “50 Cent” Jackson – $155 million
5. Bryan “Birdman” Williams – $150 million

No comments