ads

Breaking News

B’Hits yasaini wasanii wapya 3, leo yamtambulisha mmoja, yazungumzia mabadiliko inayokuja nayo

10689822_10152683677002485_4037522370647650575_n
Baada ya kimya cha miezi kadhaa, B’Hits Music Group inarejea tena na sasa ikiwa na wasanii wapya watatu.
Producer wa B’Hits, Pancho Latino akiwa na msanii mpya, Kim
CEO wa B’Hits, Hermy B, ameiambia Bongo5 kuwa kwa muda wote waliokuwa kimya walikuwa busy kutengeneza kazi mpya ambazo umefika muda wa kuanza kuziachia. Hermy amesema tayari wamechukua wasanii wapya watakaokuwa chini ya label hiyo.
“Kwa muda wote ambao tuliokuwa kimya nahisi watu walikuwa wanahisi labda sisi hatufanyi kazi, lakini muda wote ambao tumekuwa kimya tumekuwa tukifanya kazi,” amesema Hermy.
“Katika kufanya kazi, pia tumekusanya wasanii wengine ambao tunafanya nao kazi, ukimjulisha na kundi la District 9 ambao tulisema wanakuja, nao walikuwa studio muda wote huo kila mtu amekuwa akitengeneza muziki wake, album yake. Kwakuwa imekuwa ni process ya creation, process ya innovation na process pia ya kuanalyse tulipotoka na wapi tunataka kwenda.”
IMG_0096
Hermy amesema hadi sasa wameshachukua wasanii watatu wa kuanzia japo mipango ya kuongeza wasanii wengine siku za usoni ipo. “Mmoja ambaye tumeanza kumtoa ni Kim. Kim ndio tumeamua kutoa wimbo wake ambao ameshirikiana na Godzilla, unaitwa ‘Hell Yeah’
Hermy amesema mashabiki wa muziki wategemee mabadiliko makubwa kutoka B’Hits.
“Basically watu wategemee talent nzuri, creation ya vitu tofauti tofauti. Muziki wetu hautasound kama vile watu wamekuwa wakizoea zamani B’Hits. Na ukisikia hiyo nyimbo ambayo tumetoa sasa hivi tayari utakuwa umesikia utofauti kuanzia kwenye creation ya sound yenyewe mpaka kwenye quality ya sound yenyewe. So tumekaa upande wa kuhakikisha kuwa creativity iko sawa, innovation iko sawa na talent ipo juu,” ameongeza Hermy.
Isikilize hapo chini ngoma ya Kim akimshirikisha Godzilla.

No comments