ads

Breaking News

Video: Trailer ya kwanza ya Furious 7 yaonesha scenes za mwisho za Paul Walker kabla hajafariki kwa ajali

Trailer ya kwanza ya Furious 7 ilizinduliwa Jumamosi, Nov. 1 na kuonesha scenes za mwisho za marehemu Paul Walker alizofanya kabla ya ajali iliyosababisha kifo chake November 2013.


Kwenye clip hiyo ya dakika mbili na kitu, Walker aliyekuwa akijulikana kwenye filamu hiyo kama Brian O’Conner anaonekana akifanya kile alichokuwa akikipatia – mbio za magari. “Just when you didn’t think it could get any better,” anasema Walker.
“One last ride,” Vin Diesel anayetumia jina Dominic Toretto anasikika akimumbia rafiki yake huyo wa kitambo. Walker alifariki akiwa na miaka 40 kwa ajali ya gari huko Santa Clarita, Calif.
Utengenezaji wa filamu hiyo ulisimama kwa muda na baadaye kaka zake Caleb na Cody waliongezeka kuimalizia. Wengine waliogiza kwenye filamu hiyo ni Michelle Rodriguez, Jordana Brewster, Dwayne “The Rock” Johnson, Tyrese Gibson, Ludacris, Elsa Pataky na rapper Iggy Azalea.
Furious 7, itaingia sokoni April 3, 2015.

No comments