ads

Breaking News

Rich Mavoko azitaja silaha mpya za kufungia mwaka

Rich Mavoko
Baada ya kuachia ‘Pacha Wangu’, Rich Mavoko amesema yupo chimbo kuandaa silaha za kufunga
mwaka.Mavoko ameiambia Bongo5 kuwa sababu inayomfanya aachie wimbo mpya ni baada ya kuona mashabiki wa muziki wake bado wanahitaji mawe zaidi kutoka kwake.
“Kuna kazi ipo ndani imeshafanyiwa kila kitu, manejimenti wapo kwenye maandalizi kwaajili ya uzinduzi. Mimi nahisi inaweza ikatoka kufunga mwaka na pia kama tukiona vipi inaweza ikatoka kufungulia mwaka.” amesema Mavoko.
Katika hatua nyingine Mavoko amesema mwaka huu umekuwa wa neema zaidi kwake.
“Mwaka huu umekuwa vizuri sana kwenye biasahara ya muziki wangu, kwahiyo tunajipanga na kuomba Mungu mwakani uwe mzuri zaidi. Kuna mambo makubwa nimeyafanya mwaka huu lakini siwezi kuyaweka hadharani bado haijaisha. Lakini mambo yako vizuri, vikiisha watu wataviona.”

No comments