ads

Breaking News

Ni mwanamke ndiye aliyelifanya kundi la Wanaume TMK kumeguka!

pageKundi la Wanaume TMK aka ‘wazee wa mapanga shaaa’ lilijichukulia umaarufu mkubwa enzi likiwa na members wote waliolianzisha.

Hata hivyo kundi hilo lilikuja kuvunjika na kuzaliwa makundi mawili, Wanaume Halisi linaloongozwa na Juma Nature na TMK Wanaume Family ambalo lipo chini ya Said Fela likiwa na wakali kama Chege na Mheshimiwa Temba. Na sasa imebainika kuwa ni mwanamke ndiye aliyewakosanisha jamaa hao.
“Tatizo wote tulivurungwa na ujana mwisho wa siku tukatoa chance kwa watu na wamechukua nafasi,” Fela aliiambia Bongo5.
“Siwezi kusema sio au ndio, lakini huyo mwanamke ameshinda ametushawishi mpaka kubomoa, maana yake ni sawa sawa mwanamke anatumwa kwenda kubomoa nchi. Viongozi kama tunagombania nchi kwaajili ya mwanamke basi tulifeli sisi upande wetu,” alisisitiza.
Jumatatu hii Mheshimiwa Temba amepost picha ya Wanaume TMK kabla halijameguka na kuandika ‘Kabla shetani hajapita.”
Fela amedai kuwa anapanga kuzungumza na Nature ili waendelee kufanya kazi tena.

No comments