ads

Breaking News

Nameless apanga kumshtaki blogger aliyezusha anataka kumpa talaka Wahu

10451741_776822129035540_1590419930152147968_nMuimbaji wa Kenya, Nameless hana mpango wa kumpa talaka mke wake, Wahu.

Tetesi hizo za talaka zilianzishwa kwenye mtandao wa Facebook, na blogger mmoja aitwaye George Moseti, Jumapili.
Nameless amesema anapata ushauri wa kisheria kutoka kwa mawakili wake ili kumshtaki Moseti.
Akiongea kwa simu na gazeti la The Star, muimbaji huyo alisema: Maelezo ya blogger huyo yalikuwa upuuzi tu na nitatoa maelezo yangu rasmi kabla mwisho wa wiki. Huwa sijibu udaku lakini huu umeenda mbali sana.”
“Blogger huyo alivuka mipaka zaidi na kuwaingiza watoto wangu kwenye ujinga huu. Sijui alipata wapi taarifa zinazoonesha kuwa tulifanya vipimo vya DNA,” aliongeza.
“Tulikuwa na habari za aina hizo hizo lakini tuliziacha zipite. Lakini hii, tunachukua hatua na itakuwa fundisho kwa wengine wanaojaribu kuandika uongo kupata wasomaji kwenye blog zao.”
Post hiyo ilisomeka:
“I suspected this n I saw it coming: Nameless files to divorce Wahu after paternity tests proves that the second child isn’t his…”

No comments