ads

Breaking News

Macaulay Culkin (Kevin) wa ‘Home Alone’ athibitisha kuwa yupo hai baada ya kuzushiwa kifo weekend iliyopita

kevin
Muigizaji na mwanamuziki Macaulay Culkin (34) aliyepata umaarufu kupitia filamu ya ‘Home Alone’ aliyoigiza enzi za udogo wake kama Kevin, amezizika tetesi zilizoibuka weekend iliyopita kuwa amefariki dunia.

Culkin ametumia mitandao ya kijamii kuthibitisha kuwa bado yupo hai na ni mzima.
Taarifa hizo za uzushi zilianzia Facebook kupitia akaunti feki iliyoandika:

“At about 11am ET on Friday (November 7, 2014), our beloved actor Macaulay Culkin passed away. Macaulay Culkin was born on August 26, 1980 in New York. He will be missed but not forgotten. Please show your sympathy and condolences by commenting on and liking this page.”

Ukurasa huo uliondolewa muda mfupi baadae.
Mwakilishi wa Culkin alitoa taarifa rasmi weekend iliyopita ya kuthibitisha kuwa star huyo ni mzima.
“He joins the long list of celebrities who have been victimised by this hoax. He’s still alive and well, stop believing what you see on the internet,”
Culkin ambaye pia ni mwanamuziki aliamua kutumia akaunti ya bendi yake iitwayo ‘Pizza Underground’ kuthibitisha kwa kupost picha akiwa ameshika kinywaji na kuandika:
“We’re on tour you silly people”.

No comments