ads

Breaking News

Lupita Nyong’o aliwahi kuambiwa asingepata mume kama asipojichubua

1256510_723820637699839_5111991235020200352_n

Muigizaji wa filamu ya 12 Years A Slave na mshindi wa tuzo za Oscar, Lupita Nyong’o amesema alikuwa akishawishiwa kujichubua ili apate mchumba.


Alisema hayo kwenye mahojiano na jarida la Marekani la Glamour. “Ubora wa urembo wa Ulaya ni kitu ambacho huathiri dunia nzima – wazo kuwa ngozi nyeusi si urembo, kwamba ngozi nyeupe ndio ufunguo wa wa mafanikio na mapenzi. Afrika pia haikwepi hili. Nilipokuwa darasa la pili, mmoja wa walimu wangu aliniambia, ‘Utampata wapi mume? Utampata wapi mtu mweusi kama wewe?
Niliabika sana. Nakumbuka niliwahi kuona tangazo ambapo mwanamke anaenda kwenye usaili na hapati kazi. Kisha anaweka cream usoni kujichubua na kisha anapata kazi! Huu ndio ujumbe: Kwamba ngozi nyeusi haikubariki.”

Lupita alidai kuwa watu aliokuwa akiwaangalia zaidi ni mlimbwende wa Sudan Kusini, Alek Wek na malkia wa talk shows, Oprah Winfrey.

No comments