ads

Breaking News

joh Makini aelezea alikotoka mbali na Geez Mabovu, ‘Geez was my dude’Joh Makini
Rapper Joh Makini ni miongoni mwa watu walioumizwa zaidi na kifo cha rapper Geez Mabovu na ndio maana yeye na wenzake wa Weusi wameamua kuahirisha show ya Mbeya iliyokuwa ifanyike Ijumaa hii kwa heshima yake. Joh na Geez walifahamiana kitambo
.“Geez alikuwa family,” Joh
“Kipindi hata watu hawanifahamu kwenye industry, kipindi tupo MJ Records, wakati hata Master J hanitambui 2002 nadhani. Kulikuwa na familia inaitwa Machizi wa Hatari ambayo ilikuwa chini ya Profesa Ludigo. Mimi sikuwa Machizi wa Hatari, Machizi wa Hatari walikuwa Geez, Fid, Mapacha na Squeezer. Mimi nilikuwa kama msanii kutoka Arusha niliyekuwa na harakati zangu, mimi na Bonta, kwahiyo hapo ndio tukaanza kuwa marafiki na washkaji,” anasema rapper huyo.
“Geez ni mmoja kati ya wasanii wa hip hop ambao mimi nimeshirikiana nao mtaa na ghetto kwasababu niliishi Kinondoni the same street na Geez Mabovu, mimi nilikuwa naishi na Mapacha na yeye anaishi ghetto jingine tofauti kipindi ambacho wao wanaheshimiwa na tayari wana nafasi MJ Records, mimi nimekuja Dar kutafuta maisha kwenye muziki. Kwahiyo Geez is my dude mshkaji wangu sana. Kilichotuweka mbali na maisha na vitu kama hivyo.”
Rapper huyo amekumbushia kuwa enzi hizo yeye, Geez na Mapacha walikuwa wanatembea kwa mguu kutoka Kinondoni B hadi Masaki kwenye studio za Master J.
Joh anasema wimbo wa mwisho alioshirikishwa na Geez ni ‘U Can’t Stop Me Now’ ambao chorus ilifanywa na Nisher na wimbo kutayarishwa na P-Funk. “Ilikuwa ni bonge moja la dude ambalo nahisi Geez kutokana na matatizo ya kiafya na hakuwa na mtu wa kuusimamia muziki wake ile ngoma haikufanya vizuri.”
Joh anasema kutokana na kuona thamani ya wimbo huo na hakutaka upotee, alifikia kipindi cha kumuomba Geez uwe wake ili ahakikishe unafanya vizuri.
“Tulipofanya hii ngoma kwa Majani nikamwambia ‘Geez hii ngoma kali’ lakini mimi ndiye niliyekuwa namcheck sababu nilikuwa naiona ile ngoma. Nilikuwa nahisi kuna matatizo yanamsumbua au labda ni life au stress whatever. Nilikuwa nikiuangalia huo muziki niliofanya na yeye na nikiulinganisha na muziki wa hip hop uliopo kwenye mainstream, nilikuwa naona muziki mkubwa sana ndio maana nilikuwa namuambia niachie huu muziki uwe wangu ili niupush wewe uwe kama umeshirikishwa.”
Joh anasema alikuwa amejiandaa hadi kufanya video ya wimbo huo.
Joh anadai alionana na Geez Mabovu siku ya mwisho ambayo alikutana na marehemu Langa pia.

No comments