ads

Breaking News

Gosby kuachia wimbo uitwao ‘Wema Sepetu’ leo

10735393_1484974168444049_1705862547_n
Rapper Gosby leo anaachia ngoma mpya kupitia utaratibu wake wa kutoa wimbo kila Jumatano.
Wimbo huo utakaopatikana kwenye mixtape yake, Miss Tape, unaitwa ‘Wema Sepetu’. Ngoma hiyo imerekodiwa ndani ya studio za Feel Good Music na imetengenezwa kwa ushirikiano wa producers wawili, Jeffrey kutoka Marekani kwa upande wa midundo na Cjamoker kutoka Tanzania kwa upande wa recording, Mixing and Mastering.Gosby amesema ameamua kushirikisha producers wa nje na wa ndani ya nchi ili kuongeza ladha kwenye muziki wake na vilevile kupata uzoefu wa kufanya kazi na watayarishaji tofauti.
“Muziki wetu unakuwa kwa kasi kubwa, na kama mnavyojua kuwepo kwa mitandao mbalimbali ya kusambaza kazi zetu online inarahisisha sana kazi zetu kufika popote dunia, nadhani ni wakati muafaka sasa tukianza kuangalia soko hili kwa upana zaidi, kuwa na ladha ya bongo na vilevile kuweka ladha ya kimataifa pia,” amesema.
Akiongelea kuhusu wimbo huo Gosby anasema:
“Wema Sepetu, dah sijui nianzie wapi ili iwe rahisi kueleweka, anyways.. Wote tunamjua Wema au tumewahi kusikia au kusoma habari kuhusu Wema, ni former Miss Tanzania, movie star, celebrity wa kike ambao anapendwa sana na watu ndani na nje ya Tanzania. Wanawake wengi wanatamani kuwa Wema Sepetu kwa ujumla au sehemu tu, na huu wimbo umeongelea juu ya msichana au mtoto wa kike ambaye anafanana na Wema Sepetu
Sasa wimbo huu ni special kwa wasichana wote ambao wanaofanana na WEMA SEPETU ngoja nisimalize utamu, tega sikio mchana huu.”

No comments