ads

Breaking News

Fella asifia kazi mpya zijazo za Yamoto Band, ‘zikitoka utasema ni kali kuliko ulizowahi kuzisikia’

Yamoto2
Mkurugenzi wa Yamoto Band amefunguka kwa kusema kuwa Yamoto Band hawabahatishi kwenye kazi zao, huku adai kuwa kazi mpya zinazokuja ndo zitadhihirisha uwezo mkubwa wa kuimba na kutunga.

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni Fella alisema kuna nyimbo ambzo zikitoka watanzania watahisi Yamoto Band ndo inaanza upya.
“Tuna nyimbo nyingi ambazo zipo tayari na zikitoka leo utasema hii ni kali kuliko hata ulizowaizisikia, sisi hatutaki kushindana na band yoyote lakini watanzania ndo wanajua sisi tunafanya nini. Kuna nyimbo ambazo zikitoka sasa hivi utaamini kuwa Yamoto Band hawabahatishi, kuna nyimbo tatu zipo tayari tupo kwenye uchaguzi wa kujua tutoe ipi, kwahiyo wadau wakae mkao wakula ” alisema Fella

No comments