ads

Breaking News

Diamond amtaja msanii wa Marekani ambaye ana ndoto ya kufanya naye collabo

Diamond-600-x-450
Tumeshasikia kuwa kuna msanii wa Marekani ambaye Diamond Platnumz tayari amefanya naye collabo ingawa bado hajamuweka wazi, lakini hivi karibuni alimtaja msanii mkubwa wa Mareknai ambaye ana ndoto ya kufanya naye pia collabo.
Akizungumza na show ya Sporah, Diamond amesema licha ya kufanikiwa kufanya collabo na baadhi ya wasanii wakubwa wa Africa kama Davido, Iyanya, Mafikizolo na wengine, lakini ndoto yake ya miaka mingi ni kufanya wimbo na hit maker wa ‘Good Kisser’, Usher Raymond.
“Natamani nifanye wimbo na Usher Raymond sana, natamani nifanye naye nyimbo kwasababu ni mtu ambaye nilikuwa nikimtazama tangia mdogo nakua, nikifanya nae nahisi nitatimiza moja ya ndoto zangu.” alisema

No comments