ads

Breaking News

Blac Chyna amshutumu Tyga kwa ku-hack akaunti yake ya twitter na kutweet ‘I’m a gold digger and cheater’

tyga-blac-chyna
Muda mfupi baada ya Blac Chyna kuonekana ametweet kitu kilichowashtua watu wengi Jumapili asubuhi, kuwa yeye ni ‘gold digger’ ambaye alikuwa na Tyga kwa sababu ya pesa, Chyna alikanusha kuwa si yeye aliye tweet na kudai kuwa baba wa mwanae Tyga ame ‘hack’ akaunti yake.
Tweet hiyo ilisomeka, “I’m a gold digger and cheater. I never really loved Tyga It was always about the money”, ikafuatiwa na tweet nyingine, “After he took me out the strip club gave me a beautiful family. Help me one multiple business”.
blac-chyna-twitter-3
Baada ya tweet hizo, baadae Blac Chyna alitumia akaunti yake ya Instagram kutoa taarifa kuwa akaunti yake imekuwa ‘hacked’ na Tyga. Muda mfupi baadae tweet hizo ziliondolewa.
Blac Chyna alirejea kupost twitter kuwa tayari ameirejesha akaunti yake, na kutweet kuwa asingeweza kutweet vitu kama vile. Aliongeza kuwa kwa sasa anataka kushirikiana nae (Tyga) kwenye malezi ya mwanao peke yake.
tweet1
tweet2
tweet3

No comments