ads

Breaking News

TID na Dully Sykes waondoa tofauti zao, warekodi ngoma, ‘Money Girl’

Dully Sykes na TID
                                                          Dully Sykes na TID

Wakongwe wawili wa muziki wa Bongo Flava, TID na Dully Sykes wamemaliza tofauti zao na kuamua kuingia studio kufanya wimbo wa pamoja uitwao’Money Girl’Akizungumza leo na 255 ndani ya XXL ya Clouds FM, TID alisema hawana sababu ya kuendelea kulumbana kwani wana kazi kubwa ya kufanya muziki mzuri kwaajili ya mashabiki wao.
“Unajua Dully Sykes sikurekodi wimbo naye ndo tumekutana tufanye hivyo,” alisema TID.
“Dully unajua yuko na studio nzuri sana sasa hivi, so Dully the first naamini anafanya nyimbo nyingi za Bongo Flava, idea ya wimbo kwa sababu ni wimbo wangu chochote lazima niproduce, nikatengeneza chorus fulani hivi. Nilimtumia kwa idea ya chorus yeye ataenda kutengeneza beat, sasa kitu kizuri ambacho nimegundua hakutengeza beat yote, time nilivyoenda pale juzi ndo akaanza kutengeneza pale wakati mimi naimba chorus yeye anatengeza beat. Lakini bado the song is not ready, tunatengeneza kwanza demo tu halafu ndo tuitengeneze. Kuna vitu vingi vinatakiwa vifanyike. The song is called ‘Money Girl,” aliongeza.
“Mimi na Dully Sykes tulikuwa tuna bifu sababu tulikuwa na conflict za utotoni lakini kumbuka sasa hivi ni 2014, influence yetu imefanya wanamuziki wengi kufanya muziki so lazima nifanye naye wimbo. Kitakuwa kizuri kwa wote ambao wana u-support muziki wa Bongo Flava.”

No comments