ads

Breaking News

T.I adondosha album mpya ‘Paperwork’ baada ya kurejea Marekani akitokea Bongo

ti-paperwork-

Rapper T.I ambaye tayari amerejea nchini Marekani baada ya kuwarusha mashabiki wake wa Tanzania kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2014 Jumamosi iliyopita, leo October 21 ameachia rasmi album yake mpya ‘Paperwork’.
“The wait is OVER!!!!!! #PaperworOUTNOW #ItsDaKINGBiiiitch #HustleGangOverErrrrthang” T.I ameandika Instagram leo.
‘Paperwork’ ni album ya tisa ya Clifford Joseph Harris, Jr maarufu kama T.I ambayo imetolewa chini ya Grand Hustle Records na Columbia Records. Album hii ni project ya kwanza ya T.I akiwa chini ya Columbia Records baada ya kumaliza mkataba wake na Atlantic Records.
Mastaa walioshirikishwa kwenye album hii ni pamoja na Chris Brown, Rick Ross, Usher, Pharrell Williams ambaye ndiye executive producer wa album hiyo, bila kumsahau rapper wa kike Iggy Azalea aliyemshirikisha katika hit single yake ‘No Mediocre’.
Baada ya kuwasili nyumbani jana T.I aliandika:
“Just touched down. Back in the land. Already blowin #JetFuel. #PaperworkOct21 #ItsDaKINGBiiiitch #HustleGangOverErrrrthang”

No comments