ads

Breaking News

T.I. adai hawezi kulazimisha Iggy Azalea na Snoop Dogg wapendane

1413406264_iggy-ti-snoop-zoomT.I.amesema hayupo kwenye nafasi ya kuwafanya Iggy Azalea na Snoop Dogg wapendane.

Rapper huyo aliyetumbuiza kwenye Serengeti Fiesta, October 18 jijini Dar es Salaam alimshawishi Snoop amuombe radhi Iggy baada ya kumkwaza kwa kupost picha ya albino wa kike kwenye Instagram na kudai kuwa ni Iggy pasipo make-up.
“Namheshimu Snoop vya kutosha, namheshimu Iggy vya kutosha, kwa wao kutengeneza maoni ya kuheshimiana kwa yeyote. Wote nawapenda. Na pengine kadri muda unavyokwenda watapata vitu ambavyo wanavipenda na sio kugundua vile wasivyovipenda,” T.I. aliliambia jarida la XXL.

No comments