ads

Breaking News

Mo Music kuachia single mpya wiki ijayo baada ya ‘Basi Nenda’

MoHit maker wa ‘Basi Nenda’, single iliyofanikiwa kuingia kwenye orodha ya nyimbo zilizofanya vizuri 2014 kwenye Bongo Fleva, Mo Music anatarajia kuachia single yake mpya wiki ijayo.

“Nimeamua kuachia ngoma mpya sasa hivi kwasababu nafikiri ni muda muafaka” . “Watu wengi walikuwa wanataka niachie ngoma katika kipindi walichokuwa wanahitaji, lakini nikawa najifikiria kitu kwasababu ‘Basi Nenda’ ilikuja muda ambao walikuwa hawaufahamu.”
Kuhusu utofauti utakaokuwepo katika single mpya Mo amesema, “Kwanza naweza kusema midundo halafu vile vile uandishi, nimetumia techniques kubwa , nimetumia mitindio mikubwa sana ya sauti kuwaonesha Watanzania kwamba tunajua kuandika halafu na ubora wa kazi yenyewe.”
‘Simama’ ambao ameufanya kwa Mazuu ndio jina la wimbo anaotarajia kuutoa, japo amesema bado yupo njia panda sababu zipo nyimbo mbili kali ambazo mpaka kufikia wiki ijayo atakua amepata uamuzi wa mwisho wa ipi itangulie kutoka.
“Nimefanya kazi kwa Lollipop, nimefanya kazi kwa Mazuu Records, kwa Lollipop inaitwa ‘Natamani’, kwa Mazuu inaitwa ‘Simama’”.
Ameongeza kuwa hakuna msanii yeyote aliyemshirikisha kwenye nyimbo zote mbili sababu bado anahitaji kuonesha uwezo wake.
“Nataka nioneshe uwezo wangu kwanza, bado nafikiri nina uwezo mkubwa kuweza kusimama peke yangu japokuwa tayari nina wigo mkubwa sana kuweza kumshirikisha mtu yeyote, lakini nimeona tu kwamba nioneshe bado nina uwezo wa kusimama mimi mwenyewe.”
Kuhusu amejiandaaje kubaki mahali ambapo Basi Nenda imemfikisha au juu zaidi yake, Mo Music amesema, “Kwanza ndio maana nikakaa muda kidogo kuweza kujipanga niweze kujua ni wapi ambapo kuna mapungufu ambayo natakiwa niyapunguze, wapi ambapo niongeze, lakini kikubwa ni mipango na mbinu ambazo tumeziandaa mimi na mtu ambaye tunashirikiana katika swala la muziki. Pia naahidi kufanya video kubwa sana.”

Mo Music ni miongoni mwa wasanii ambao walipata nafasi ya kuzunguka kwenye tour ya tamasha kubwa la Fiesta 2014, ambalo Jumamosi hii linatarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam ambapo rapper wa Marekani T.I anatarajiwa kushare jukwaa na wasanii wa Bongo.

No comments