ads

Breaking News

Kila baada ya miezi 3 ni ngoma, na kila miezi 6 ni video mpya – Cpwaa

cpwaa2
Rapper Cpwaa ambaye hivi karibuni aliachia single yake mpya ‘Kata Kiu’ amesema label yake Brainstormusic inatarajia kuongeza wasanii na kuanza kufanya filamu pamoja na kuanza kutoa ngoma nyingi zaidi.
Cpwaa amesema kuanzia sasa atakuwa akatoa nyimbo nyingi ili kuwapa mashabiki wake muziki wa kutosha.
“Baada ya hii ‘Kata Kiu’ kabla mwaka huu haujaisha nitatoa single nyingine kwahiyo sasa hivi ni nonstop, kila baada ya miezi mitatu nitakuwa natoa nyimbo na kila baada ya miezi sita natoa video, that’s my target now,”  “Kwasababu nimekaa muda mrefu bila kufanya kazi kwa wingi, kwahiyo hii ‘Kata Kiu’ ni kwaajili ya kukata kiu mashabiki wangu ambao wamemiss kitu fulani. Kwahiyo huu ni wimbo ambao unagusa kila level, nimerudi kwenye style yangu ya zamani watu wana hamu nayo pia Chereko Chereko bado inaendelea kwenye rotation,” alisema Cpwaa.
Cpwaa amesema pia label ya Brainstormusic itaongeza msanii mpya pamoja na kuingia kwenye filamu.
“Kuna kampuni kama tatu ziko interested na Wadananda, sasa hivi bado tupo kwenye mazungumzo ndo maana sitaki kuzungumzia sana, pia kutakuwa na TV show ambayo itakuwa accessible kwenye mobile phone. Kuna nyimbo mpya ya Mdananda itatoka na pia kuna filamu itakuja. Kwahiyo kuna mipango mingi inakuja kuhusu hii record label. Kingine kuna msanii mpya kabla ya mwaka huu haujaisha itamsaini msanii mpya na ni mkubwa wa hapa nyumbani,” alisema Cpwaa.

No comments