ads

Breaking News

Kanye West apanga kuhamia Paris na mwanae North, hata kama Kim Kardashian akikataa

north-kanye
Kanye West anadaiwa kuwa na mipango ya kuhamia (kimoja) jijini Paris, Ufaransa mwakani na mwanae North, hata kama mke wake Kim Kardashian akikataa kuhama nao.

Kim na Kanye wanadaiwa kuwa kwenye malumbano kwa muda mrefu kuhusiana na uamuzi huo.
Mtandao wa Radar online umeripoti kuwa kabla ya sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Kim iliyofanyika, Tao Nightclub, Las Vegas wawili hao walijikuta wakilumbana kuhusiana na jambo hilo.
“Wakati wanajiandaa, Kanye alimuambia Kim kwa upole kuwa anapanga kuhamia Paris… na amepanga kufanya hivyo bila yeye (Kim). Ilikuwa kama ngumi nzito nyuma ya kichwa chake,” kilisema chanzo kimoja.

No comments