ads

Breaking News

Filamu ya maisha ya Aaliyah kufichua undani wa uhusiano wake na R.Kelly

Baada ya pilikapilika na ukosoaji wa hali ya juu kuhusu uandaaji wa filamu ya maisha ya Aaliyah, hatimaye mambo yameiva na kilichobaki ni kuipakua.

Mtayarishaji wa filamu hiyo, Wendy Williams ameweka wazi kuwa filamu hiyo haitazungumzia tu maisha ya muziki ya Aaliyah bali itachimba kwa undani kufahamu mengine yanayohusu maisha yake ikiwa ni pamoja na uhusiano wake na R. Kelly suala lililokuwa gumzo.
Katika mahojiano aliyofanya na Orlando Sentinel kuhusu filamu hiyo, Wendy Williams alieleza vitu alivyotaka viwemo kwenye filamu hiyo.
“Nataka kusikia kuhusu R. Kelly. Nataka kusikia kuhusu Missy Elliot,” alisema Windy.
Nataka kufahamu alichosema baba yake pale Aaliyah mwenye miaka 16 alipompeleka nyumbani kwao mwanaume mwenye miaka 28 (R.Kelly). Nataka kufahamu alichokisema mama yake. Nataka kufahamu kaka yake alisema nini. Aaliyah alianza vipi? Na kwa kiasi gani hii kitu ya R.Kelly iliathiri kazi yake ya muziki?” Aliongeza.
Filamu ya Aaliyah iliyopewa jina la Aaliyah: The Princess of R&B inasubiriwa kwa hamu huku trailer yake ikionesha Alexandra Shipp akifanya vizuri kuvaa uhusika wa Aaliyah.
Filamu hiyo imepangwa kutoka November 15.

No comments