ads

Breaking News

Belle 9 hataonekana kwenye video ya wimbo mpya alioshirikishwa na Young Killer na Fid Q ‘13’, Msodoki atoa sababu

Belle
Wimbo mpya wa Young Killer Msodoki aliomshirikisha kaka yake kiumri na kimuziki Fareed Kubanda aka Fid Q na Belle 9, ‘13’ umetambulishwa rasmi leo (Oct. 31) kwenye vituo mbalimbali vya radio.
Habari njema kwa mashabiki wa Msodoki ambao wameupokea vizuri wimbo huo ni kuwa video ya ‘13’ iliyoongozwa na director Nisher pia imekamilika, na inatarajiwa kutoka soon. Lakini habari mbaya kuhusu video hiyo ni kuwa Belle 9 ambaye amesikika kwenye kiitikio cha wimbo huo hataonekana kabisa kwenye video.
10731754_669791816461823_711395622_n
Msodoki amekanusha maneno yaliyopo mtaani kuwa walishindwa kuelewana na Belle hadi kushindwa kutokea kwenye video hiyo.
“Hayo ni maneno sidhani kama ni kweli” amesema Young Killer kupitia Power Jams ya East Africa Radio, “kwasababu Belle ni mtu ambaye tuko nae na hii ngoma imefanyika kama wiki mbili nyuma, na baada ya kufanyika wiki mbili nyuma zikapita siku mbili tukafanya video. Kwahiyo ndani ya wiki mbili nyuma ukitoa siku mbili hizo tulikuwa nae Bongo records tumefanya ngoma, lakini ni time ambayo ilikosekana kutokana na yeye pia alikuwa katika kutambulisha wimbo wake wa Vitamin Music, so tour zake za media nadhani kidogo zilikuwa zimebanana”.
Msodoki ameongeza kuwa hadhani kama kutokuwepo kwa Belle 9 kama kutaiathiri kwa vyovyote video yake.
“Kitu ambacho naamini itatu affect kwa mawazo lakini tukiwa tunaitazama naamini watu wote tuta enjoy kutokana na sauti yake ipo na yeye pia tumem mention”.

No comments