ads

Breaking News

Video ya ‘Mr. Nay’ yamfanya Nay wa Mitego aitwe na mama yake mzazi


Screen Shot 2014-09-03 at 3.55.01 AM 
Nay wa Mitego msanii wa bongofleva ambae amethibitisha kwamba Mama yake mzazi amemuita na kutaka kujua kilichoonekana kwenye video yake mpya ya ‘Mr. Nay’ aliyoifanya Kenya kinamaanisha nini.

Screen Shot 2014-09-03 at 3.30.10 AM
Nay ambae kabla ya kufanikiwa kimuziki aliwahi kuwa kinyozi wakati bado akisoma sekondari,amesema mama yake mzazi amemuita nyumbani September 2 2014 kutaka kujua kinachoendelea sababu alichoona na anachoambiwa na watu kimemfanya apate wasiwasi mkubwa.
Nay anasema ‘mimi nafanya kitu kutokana na idea ambazo huwa zinatoka kichwani mwangu, nafikiri watu wameona ni video kubwa nzuri na kali…. sijawahi kufanya video kali kama hii ambayo kidogo inataka kuniletea shida ila sio kitu kibaya kwangu’
Screen Shot 2014-09-03 at 3.30.24 AM‘Zile damu, na vitu vingine kama vya kishetani pamoja na namba ninayopenda kuitumia ya #966 ni vitu vinavyofanya nipate sana msg na kuulizwa maswali, na ndivyo vitu vimemshtua mama mpaka akaniita, watu wengine wanadhani mimi ni mwabudu shetani ila nataka watu watambue kwamba hakuna kitu kama hicho, ni ubunifu tu… na hii namba kuna siku nitakuja kuielezea maana yake 
Screen Shot 2014-09-03 at 3.30.32 AMNay amesema ataweka wazi kila kitu alichoambiwa na mama yake baada ya kukutana nae kuzungumza kuhusu hii video ambayo imemuhuzunisha kama mzazi ikiwa ni video ya kwanza kumfanya amuite na kuhoji.

No comments