ads

Breaking News

Pistorius kukwepa kifungo cha miaka 25 Jela wiki hii?

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius amerejea mahakamani leo ambapo wiki hii atafahamu uamuzi wa mahakama kuhusu kesi ya mauaji inayomkabili.
Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Thokosile Masipa, Oscar anatuhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao mwaka jana.
Mwendesha mashitaka ameendelea kusisitiza kuwa Oscar alimpiga risasi mpenzi wake huyo baada ya kutokea ugomvi kati yao uliohusisha wivu wa mapenzi.
Katika utetezi wake, Oscar Pistorius amekiri kumpiga risasi Reeva lakini amedai kuwa alidhani ni mtu aliyevamia nyumbani kwao usiku ule.
Kesi inaendelea na Jaji Masipa kutoa maelezo ya ufafanuzi wa mwenendo wa kesi hiyo kuelekea maamuzi. Endapo Oscar atapatikana na hatia anaweza kukumbwa na adhabu ya kifungo cha miaka 25 jela.

No comments