ads

Breaking News

Mabeste: Nachaji shilingi milioni 4 kwa package nzima ya wimbo ninaomwandikia msaniiYoung D na Mabeste
Msanii wa zamani wa B’Hits, Mabeste amesema anatoza shilingi milioni nne kumwandikia wimbo msanii.
Msanii huyo ambaye ameandika wimbo mpya wa Jux, Sisikii, amesema anapouza wimbo aliondika yeye, msanii huwa na kazi ya kurudia kila alichokiimba yeye.
“Kazi ya msanii ni kukariri tu, huongezi chochote kwakuwa mimi nakuwa nimekamilisha kila kitu,” Mabeste ameiambia Bongo5. Rapper huyo amesema anatoza kiasi hicho kikubwa kwakuwa kama msanii ataweza kulipa kiasi hicho cha fedha basi atatumia nguvu nyingi zaidi kuupromote na pia hiyo ni bei kwa wasanii wakubwa na sio kwa wasanii wanaoanza.
“Ninapomuambia msanii anilipe milioni nne ni kwamba hiyo track nikimpa nakuwa nimempa moja kwa moja,” amesema Mabeste na kueleza kuwa hatahitaji fedha nyingine tena hata kama wimbo huo ukimpa mamilioni ya shilingi msanii.
Hata hivyo Mabeste amesema alilipwa shilingi milioni mbili kuandika wimbo wa Jux.

No comments