ads

Breaking News

Lil Kim awasha taa ya kijani ya Mixtape yake 'Hard Core'

Baada ya subira ya mwaka mzima, hatimaye Lil Kim ameonesha ishara ya mwendo wa kutoka rasmi kwa mixtape yake ‘Hard Core’ kwa kuachia kava ya kuitambulisha . Mixtape hiyo imechelewa sana kutoka tangu alipoitangaza July, 2013 lakini hapa katikati amekuwa na mengi yaliyomkwamisha ikiwa ni pamoja na muda wa ujauzito hadi kujifungua.
Hard Core imetoka rasmi jana. Ni mixtape yake ya kwanza tangu alipotoa Black Friday mwaka 2011.
Mwezi uliopita, Lil Kim alitoa remix ya wimbo wa Beyonce ‘Flawless’ na kumrushia makombora Nicki Minaj aliyemtaja na baadae akatoa remix ya wimbo wa Iggy Azalea ‘Fancy’.

No comments