ads

Breaking News

Joh Makini aitaja changamoto inayowakabili wasanii wakubwa na jinsi yeye anavyokabiliana nayo


Makini
Joh Makini amedai kuwa uwezo wa kuendelea kushikilia nafasi ya juu katika muziki ndio changamoto kubwa zaidi inayowakabili wasanii wengi.

Rapper huyo kutoka Arusha, amesema kutumbuiza show nyingi kwa muda uliosogeleana si changamoto kwake kwakuwa pamoja na kupata fedha, kutumbuiza ni kitu anachokipenda zaidi.
“Challenge ni kwamba unataka uendelee ku-maintain hiyo level kwahiyo inabidi uendelea kuwork hard kwasababu show haziji kama haufanyi kazi. Kwahiyo unafanya kazi, unakuwa na discipline kwenye kazi, mawasiliano mazuri na watu,”

No comments