ads

Breaking News

G-Nako kuachia ngoma mbili kwa mpigo Jumanne ijayoGnako Insta
Rapper wa kampuni ya Weusi, G-Nako anatarajia kuachia ngoma mbili kwa mpigo Jumanne ijayo.
Awali ya hapo rapper huyo aliwahi kuiambia Bongo5 kuwa yupo kwenye njia panda kuamua wimbo wake mpya wa kuachia kwakuwa amerekodi nyimbo nyingi na kali.
Kutokana na hali hiyo, rapper huyo wa Arusha alisema anafikiria kutumia watu wengine wamsaidie kuamua wimbo gani anaofaa kuutoa. “Mimi mwenyewe kama nimepagawa fulani, nafikiria kuwa na kamati kunisaidia kuamua ngoma gani natoa maana mimi mwenyewe zinanichanganya,” alisema G-Nako.
Rapper huyo alisema hadi sasa amerekodi nyimbo tano mpya na bado anaendelea kurekodi katika studio mbalimbali. Aliwataja watayarishaji aliofanya nao kazi kwenye nyimbo hizo kuwa ni pamoja na Chizan Brain, Paul Beatz na Nahreel.

No comments