ads

Breaking News

Diamond, Vanessa Mdee na Msechu watajwa kuwania ‘All Africa Music Awards

10355398_1453349568240483_3407190442092469189_n
Diamond Platnumz, Vanessa Mdee na Peter Msechu wametajwa kuwania tuzo za ‘All Africa Music Awards’ AFRIMA 2014 huko Nigeria.

Vanessa ametajwa kuwania vipengele viwili ambavyo ni ‘Msanii Bora wa kike Afrika Mashariki’ pamoja na ‘Best African RNB Soul’ kupitia wimbo wa ‘Come Over’. Diamond ametajwa kuwania Msanii Bora wa kiume Afrika Mashariki pamoja na Peter Msechu ( kwa wimbo wake Nyota aliomshirikisha Amini) na BEST AFRICAN COLLABORATION.
Upigaji kura unatarajiwa kuanza Jumanne ya wiki ijayo September 30 na tuzo zitatolewa November 9, 2014.
Vanessa ameshare furaha yake na kuwashukuru mashabiki kwa kuandika:
“Just found out I got 2 @AFRIMAWARDS nominations! #BestFemaleEastAfrica #BestAfricanRNBSoul #Tanzania #Africa ASANTE I’m over that moon.”
Ingia hapa kupata orodha kamili ya nominees
Diamond Platnumz ametajwa kuwania tuzo za ‘All Africa Music Awards’ AFRIMA 2014.
wpid-wema-akiwa-pembeni-kumsupport-diamond1.jpg
Majina hayo ya wasanii watakaowania tuzo hizo mwaka huu yalitangazwa Jumanne hii, September 23, 2014 Protea Hotel Leadway, Maryland Estate, Lagos, Nigeria. Tofauti na tuzo zingine, wasanii wanatakiwa kuwasilisha kazi zao kwa jopo la AFRIMA ambapo kazi hiyo ilianza May 15 na kufungwa July 21. Jumla ya kazi 2,025 zilipokelewa kwa uchambuzi.
Jopo la majaji wa AFRIMA ambalo linaundwa na wadau wa muziki barani Afrika, walikuwa jijini Lagos, kuanzia July 31 hadi Aug. 6 kuchambuzi kazi hizo.

No comments