ads

Breaking News

Bob Junior azungumzia collabo zake na Ben Pol na Jose Chameleone


IMG-20140819-WA0003
Rais wa Masharobaro nchini, Bob Junior amefanya collabo mbili tofauti na Ben Pol pamoja na msanii wa Uganda, Jose Chameleone.
Bob Junior ambaye hivi karibuni aliachia kazi yake mpya iitwayo Bolingo, alidai kuwa lengo la kushirikisha wasanii hao ni kuja na muziki mpya ambao watu hawajazoea kutoka kwake.
“Kuna project ya mimi na Chameleone ambayo inayoka mwezi wa 10 so bado sijajua kama itatangulia ya Ben Pol na mimi au ntatoa ngoma yangu mimi peke yangu au ya mimi na Chameleone,” alisema.
Hivi karibuni muimbaji na mtayarishaji huyo wa muziki alisema kuwa amebadilisha jina la studio yake kutoka Sharobaro Records na kuwa Sharobaro Music na kwamba muziki atakaokuwa anatayarisha utakuwa na ladha tofauti.

No comments