ads

Breaking News

Tundaman aelezea ujio wake mpya, "ni mahadhi ambayo hayajasikika mwaka huu"

Mwimbaji wa Tip Top Connection, Tundaman ameelezea ujio wake mpya kwenye game baada ya Msambinungwa kufanya vizuri.
Akiongea na Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm, Tundaman ameeleza kuwa anajipanga kuachia wimbo wake mpya unaoitwa Itakula Kwako au Temana na Mimi uliotayarishwa na Mensen Selekta.
“Walikuwa wanabishana hapa…majina Tale anasema Itakula Kwako, Madee anasema Achana na Mimi, Bonge anasema achana na mimi. Kwa hiyo jina linaweza kuwa itakula kwako au achana na mimi.” Amesema Tundaman.
Akiuelezea wimbo huo, mwimbaji huyo amesema kuwa ni wimbo wenye ujumbe wa mapenzi ambao unawataka watu kuwa na mtu mmoja wanaempenda kati ya wengi walionao.
“Ni wimbo ambao unazungumzia mapenzi katika hali tofauti kidogo kwa sababu sasa hivi kila mtu anakuwa na wanawake wawili au watatu, au mwanamke anakuwa na wanaume wawili au watatu. Kwa hiyo inafika time inabidi tuwe wakweli. Kwa hiyo nimezungumzia ukweli kwamba mimi nina wanawake kama watatu lakini nawaambia wengine kwamba waachane na mimi kwa sababu kuna mmoja ambaye ninampenda.”
Amesema wimbo huo utakuwa na mahadhi ambayo hakuna msanii ambaye ameyagusa mwaka huu.
“Ni mahadhi fulani hivi kama chakacha, kama mdundiko yaani kama…sijui nisemeje. Ni ngoma fulani ambayo ukiisikia iko tofauti na beat ambazo…hujawahi kusikia toka mwaka huu uanze. Ni ngoma fulani hivi sio speed sana ila ni ngoma fulani ya kuchezeka lakini sio speed sana kama Msambinungwa.”

No comments