ads

Breaking News

Muigizaji mwingine maarufu wa Marekani 'Lauren Bacall' afariki

Siku moja baada ya kufariki muigizaji maarufu wa Marekani Robin Williams kufariki, tasnia ya filamu ‘Hollywood’ imepata pigo jingine kubwa baada ya muigizaji wa kike Lauren Bacall kufariki akiwa na umri wa mika 89.
Muigizaji huyo ambaye aliigiza filamu zaidi ya 30 ikiwemo The Mirror Have Two Faces, How to Marry a Millionaire, To Have and Have Not amefariki jana (August 12) kutokana na ugonjwa wa kiarusi uliomsumbua kwa muda mrefu.

Lauren Bacall miaka ya 1940

Kupitia akaunti ya Twitter inayoendeshwa na mtoto wa Bacall imeandikwa tweet ya kuthibitisha kifo chake.
“With deep sorrow, yet with great gratitude for her amazing life, we confirm the passing of Lauren Bacall.”
Bacall amewahi kushinda tuzo ya Golden Global na kutajwa kuwania tuzo za Oscar. Mwaka 1999 alishika nafasi ya 20 katika orodha ya wasanii 25 wa kike (AFI’s 100 Years).

No comments