ads

Breaking News

Msanii wa Bongo Flava alizwa na 'Godzilla fake' wa Facebook

Mitandao ya kijamii inawaleta watu pamoja na kurahisisha mawasiliano, lakini mtandao huu umekuwa sehemu rahisi pia ya watu kulizwa kwa utapeli au usaliti.
Msanii mpya wa Bongo Flava aliyejitambulisha kwa jina la Cyju, Jumatatu wiki hii alifikisha malalamiko yake kupitia kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm kuwa rapper wa Salasala Godzilla amemzulumu pesa yake aliyomlipa kwa ajili ya kufanya nae collabo.
Cyju ameeleza kuwa aliwasiliana na Godzilla Facebook, kwenye ukurasa wa mtu anaejiita ‘Godzillah Golden Kingzilla’ na baadae wakapeana namba za simu ili wakamilishe zoezi huku akimuomba 250,000 kama malipo ya collabo hiyo.
Cyju anasema baada ya mazungumzo marefu kwa njia ya simu jamaa alimpunguzia hadi shilingi 50,000. Na bila hiana jamaa alijichanga na kumtumia mtu huyo huku akimsisitiza kuwa asimuangushe. Lakini siku ya siku jamaa aligeuka na kukata mawasiliano baada ya kupewa mkwanja.
“Eid Pili nikampigia sasa asubuhi. Ikawa inaita simu hapokei..nikapiga tena hapokei. Kumcheck whatsapp kanibroke. Nikaamua kuingia FB nikamuuliza kwa hiyo Zilla ndo umenizingua? ‘Akanijubu hamna mdogo wangu’. Nikamuuliza ‘ila’..hakujibu tena na ndio mpaka hivyo.”
The Jump Off ilimtafuta Godzilla halisi na kumueleza mkasa huo ambapo alieleza kuwa hajawahi kabisa kuwasiliana na Cyju na kwamba ameshapata malalamiko mengi kuhusu huyo Godzilla fake anaechukua pesa za wasanii kwa madai ya kufanya nao collabo.
“Kuna jamaa mmoja anatumia jina langu facebook anajiita ‘Godzillah Golden Kingzilla ’. Anawaibia sana watu, na wengi wameshalalamika sana. Mimi natumia ‘King Zilla From Salasala’  . sasa muulize alikuwa anachat na akauti gani. Halafu muulize mtu aliyekuwa anachat nae kama ana namba kama hii tunayoongea na wewe.” Alisema Godzilla.
Ukweli ni kwamba Cyju alitapeliwa na mtu huyo aliyegeuza jina la rapper Godzilla wa Salasala kuwa kitega uchumi chake. Namba aliyoionesha Cyju sio namba halisi ya rapper huyo.
Shtuka, hakikisha unaewasiliana nae Facebook unamfahamu kabla ya kufanya nae biashara yoyote…hata kuanzisha nae uhusiano

No comments