ads

Breaking News

Michepuko: Mariah Carey na Nick Cannon wako mbioni kuachana

Mariah Carey na mumewe Nick Cannon wanaweza kuachana hivi karibuni kama hawataweza kushinda jaribu la michepuko linaloitikisa ndoa yao.
Vyanzo vimeiambia PageSix kuwa wanandoa hao hivi sasa wanagombana sana na wamefikia hatua ya kutengana na kwamba Nick Cannon anaishi hotelini.
“Nick Cannon haishi nyumbani kwao hivi sasa, anaishi hotelini. Wanagombana sana.” Kimesema chanzo kimoja.
Chanzo kingine kimeeleza kuwa Mariah Carey amechoshwa na tabia za Nick Cannon kuwa na michepuko mingi kiasi kwamba aliwatuma walinzi kumuangalia akae mbali na warembo wakati wa pool party iliyofanyika Las Vegas ambapo mumewe alikuwa mshereheshaji.
Mariah hakutaka kabisa mumewe anywe pombe katika party hiyo kwa kuwa alijua huingia katika matatizo baada ya kunywa.
Mariah na Nick walifunga ndoa mwaka 2008

No comments