ads

Breaking News

Baba yake Beyonce afichua siri ya tetesi za talaka kati ya Jay Z na Beyonce, Bey aripotiwa kuwa mjamzito


Baba yake Beyonce Knowles, Mzee Mattew Knowles afichua siri ya kuwepo ripoti kuwa mwanae anataka kuachana na Jay Z huku akigusia pia kuhusu kilichosababisha ugonvi kati ya Solange na Jay ndani ya lift.
Katika mahojiano aliyofanya na Roula &Ryan Show wiki hii, Mzee Mattew alieleza kuwa anachofahamu ni kwamba tetesi hizo za talaka ilikuwa mbinu ya kuuzia tiketi zaidi za tour yao.
Ameeita mbinu hiyo kuwa ‘Jedi Mind trick’ ambayo maana yake ni nguvu ya kucheza na akili ya watu kwa kutengeneza utata fulani ili kuwafanya wafikirie unachotaka kwa maslahi yako (kucheza na fikra zao).
“I know, because we’ve done this. From experience, there’s a tour going on,So you sometimes have to ignite that tour. It’s called a Jedi mind trick. The Jedi mind trick fools you a lot.” Amesema.

Alipoulizwa kuhusu ugomvi kati ya Jay Z na Solange, mzee huyo aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa ile yote inaweza kuwa trick ambayo imewasaidia pia katika tour hiyo hiyo na imesaidia kuuza albam ya solange kwa asilimia kubwa.
“All I know is the Jedi mind trick. Everyone’s talking about it. Ticket sales went up. Solange’s album sales went up 200%!”
Katika hatua nyingine, jarida la OK limeripoti kuwa Beyonce ni mjamzito tena hivyo wawili hao wanatarajia kuwa na mtoto wa pili.
Kwa mujibu wa chanzo chao, tangu mwezi mmoja uliopita Beyonce amekuwa akichagua vyakula kama alivyokuwa anafanya wakati anaujauzito wa Blue Ivy na kwamba Jay Z amekuwa akihakikisha kwamba hapati stress yoyote.

No comments