ads

Breaking News

Aunt Ezekiel: Sidhani kama Wema ni mtu wa kufundishwa...ana maisha yake

Aunt Ezekiel ambaye ni rafiki wa karibu wa Wema Sepetu, amejibu kauli ya Diamond Platinumz kuwa Wema ana marafiki wanaomfundisha tabia mbaya na kwamba kama anataka kuendelea aachane nao.
Akiongea na Bongo5, Aunt Ezekiele ameeleza kuwa anachofahamu Diamond aliongea kwa niaba ya watu walio karibu nae na hakumtaja yeye kwa jina. Lakini hata kama angemtaja yeye hadhani kama Wema ni mtu wa kufundishwa.
 “Wema ni mtu mzima anaishi mwenyewe na ana maisha yake sidhani kama ni mtu wa kufundishwa. Wema ni mtu ambaye ana maamuzi yake, watu hawajui kuna wakati wa kazi na kuna wakati wa kuspend maisha. Kwahiyo mimi na muda wangu wa kazi na nina muda wangu wakuspend.” Amesema.
Aunt Ezekiel hajali kinachosemwa na watu kuhusu ukaribu wake na Wema na kinachoendelea katika kazi zake.
“Sihitaji kuangalia kuna mtu anafuatilia maisha yangu kwamba eti nakuwaga na Wema. Hawanisaidii chochote. Nachotakiwa kuangalia nafanya kazi zangu na maisha yangu yanaenda mbele na sitaangalia watu wanasema nini. Mimi nina kazi zangu. Sijui kama Wema kama anahitajika kubadilika kwa sababu Diamond ndiyo anajua mapungufu ya Wema na Wema anajua ya Diamond.”

No comments