ads

Breaking News

R Kelly akwepa maswali, ni kuhusu mtoto wake kubadilisha jinsiaMwanamziki wa Marekani Robert Kelly maarufu kama R.kelly amekataa kujibu maswali yanayomhusu mtoto wake wa kike Jaya kubadilisha jinsia.kuwa wa kiume R Kelly amekuwa akikwepa kujibu maswali hayo juu ya hatua ya mtoto wake mwenye umri wa miaka 13 aliyotangaza kupitia mitandao ya kijamii kuwa amebadilisha jinsia yake na kuwa wa kiume akijiita Jay Kelly.Mwanamuziki huyo maarufu kutoka nchini Marekani amesema kuwa hatopenda kulizungumzia suala hilo la mtoto wake kujibadili jinsia na kuongeza kuwa hata kama kuna ukweli wowote hatovipa vyombo vya habari uhuru wa kuzungumzia.R Kelly ameongeza kuwa ni vyema watu wakaamini wanachokiona kwa macho kuliko wanachosikia kwani hata yeye amesikia juu ya suala hilo lakini si kweliR Kelly amebarikiwa kuwa na watoto wengine wawili Joann Kelly na Junior Robert Kelly aliozaa na mke wake wa zamani Andrea Kelly.

No comments